Nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa hapo baadaye. Nafanya juhudi ili kutimiza ndoto yangu. Sikupotea katika lengo langu. Naitwa Leah Anderson, mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu niliyezaliwa miaka 24 iliyopita hapa Njombe.
Nimekulia Mbeya ambako wazazi wangu walikuwa wakiishi. Baada ya kumaliza elimu ya msingi sikufanikiwa kuendelea kwani sikufaulu hivyo nikajitosa uraiani. Wazazi wangu walifariki nikiwa shule ya msingi hivyo nikawa nalelewa na mama mkubwa. Mwaka 2003 mama yangu mdogo ambaye ni mwalimu Sumbawanga, alinipeleka huko na akanilipia kusomea ushonaji nguo. Nikasoma kwa muda wa mwaka mmoja na kuhitimu mafunzo hayo. Sikuishia hapo mwaka 2007, mama yangu mkubwa alinilipia kusoma masomo ya sekondari na nikasoma kwa muda wa miaka miwili. Nilifanya mtihani wa kufuzu elimu ya sekondari unaoitwa ‘Qualifying Test (QT)’. Bahati mbaya sikufaulu. Wazo la kutimiza ndoto yangu ya utotoni likanijia na niliomba mtaji wa biashara kutoka kwa mama mkubwa na akanipatia kiasi cha shilingi 60,000. Nikaanza kununua nguo na kutembeza mtaani nikisaka wateja.
Lengo langu lilikuwa ni kukuza mtaji hivyo nilianza kutenga faida na baadaye nikapata wazo la
kufuga kuku wa kisasa. Kwa kuwa biashara niliyokuwa nikifanya ya kuuza nguo haikuwa ikiniingizia
pesa za kutosha, nilimuomba mama aniongezee mtaji ili ninunue kuku wa kisasa. Mama alifurahi kwa kuwa aliona kuwa nilikuwa na nia ya kuendelea na akaniongezea shilingi 100,000 nami nilikuwa na shilingi 50,000 nikanunua kuku 20 nikaanza kufuga. Wale kuku 20 walipokomaa nikawauza. Novemba mwaka 2009, nikanunua vifaranga 50 kwa kila mmoja shilingi 3,000. Mwezi wa tano mwaka huu nikaanza kuokota mayai na kuuza.Mayai nayauza kwa trei moja shilingi 4,500 na kila yai ni shilingi 200. Kwa mwezi naweza kupata kwa wastani shilingi 135,000.
Najivunia kuwa mpaka sasa najitegemea katika mahitaji madogo ambayo hapo
mwanzo nilikuwa nategemea kupewa na mama. Nina mtoto mmoja ambaye kwa sasa anasoma na namsomesha mwenyewe. Matumizi yangu siyo makubwa sana isipokuwa ni kumlipia mtoto wangu ada ya shilingi 50,000 na kujikimu mwenyewe katika mahitaji muhimu. Bado napigania lengo langu baadaye niwe mfanyabiashara mkubwa wa kuuza nguo na viatu. Kujiendeleza kielimu ni wazo lenye kipaumbele kwangu. Kwa kuwa maisha ni malengo, natarajia kuwa na watoto watatu Mungu akinijalia.Vilevile, napenda sana michezo hasa mpira wa miguu na kuimba.
Muda wangu mwingi ni katika shughuli zangu za biashara na jioni nahudhuria mazoezi ya kuimba kanisani.Nawashauri vijana wajishughulishe katika kazi mbalimbali na kuondokana na wazo la kutegemea wazazi au ndugu kwani bila ushirikiano wako, utajikuta ukiwa na
maisha magumu na kushindwa pa kuanzia. Natambua kuwa magonjwa ya maambukizi kama Ukimwi ni tishio kubwa duniani, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuchukua tahadhari ya kujilinda kwa kuepuka mazingira yanayoashiria kukuingiza katika mambukizi mapya.
Like everything in life, we gain more by working together. This page is produced as a partnership between three organizations working in Tanzania to promote open talk and healthy lifestyles
Thursday, January 13, 2011
Ruka Juu
Kuanzia Machi 2011 kwa wiki 11 mfulilizo. Kila wiki saa moja ya kuburudika, kujifunza na ku’feel ‘ maisha halisi ya washiriki. Ni shindano la wajasiriamali wachanga kutoka pande tofauti za Tanzania. Ni Ruka Juu na Fema TV Talk Show, katika vituo vya ITV na TBC1. Kuwa mmoja wa Watanzania milioni 3.4 wanaotarajiwa kuliangalia kila wiki! Ruka Juu , shindano la wa jasiriama li katika runi n ga . Jiu nge nasi na washiri ki 6 amba po wa tashindana kup ata shi lingi milioni 5 kwa ajili ya kuwek eza k wenye bia shara za o. On esho lim eja a sh angwe n a matukio kibao ya ku shtukiza! Usikose! IT V Jum amosi 12 : 30 – 1:30 Jioni TBC1 Jumap ili 3:00 – 4:00 Usiku
Subscribe to:
Posts (Atom)

